AZAM HATA WAKITAKA TUKACHEZE KIWANDANI, TUKO TAYARI – MANARA


Simba kupitia kwa afisa habari wake Haji Manara imesema ipo tayari kucheza popote watakapochagua Azam kwa sharti la kufuatwa kwa sheria na kanuni za soka.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu Tanzania bara iliyotoka mwezi wa July, mchezo wa Simba vs Azam unapaswa kuchezwa kwenye uwanja wa taifa huku Azam FC wakiwa wenyeji wa mchezo huo.

Kutokana na kuwepo kwa mchezo wa kimataifa kati ya Serengeti Boys dhidi ya Congo Brazzaville, mchezo wa Azam vs Simba umehamishiwa kwenye uwanja wa Uhuru.

Azam FC umetaka mchezo huo uwatambue Simba kama ndiyo timu mwenyeji huku wakitaka mchezo wa marudiano uchezwe kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi kitu ambacho kimeifanya Simba waibuke na kutoa kauli yao.

“Niliwaambia sio Chamazi, kokote pale ikiwezekana tucheze kiwandani Pugu au Vingunguti kama inaruhusiwa na kama kuna uwanja mule ndani tutakwenda kucheza ilimradi mechi ichezwe kwa kufuata sheria 17 za mchezo wa soka”, Manara aliiambia Azam TV.

“Hatuwezi kukaa kushinikiza nani awe mwenyeji mwisho wa siku baada ya dakika 90 mshindi anapatikana, kwahiyo sisi kazi yetu sio kupanga ratiba nani anachezea uwanjani gani.”

“Mimi binafsi leo ukiniuliza, sioni sababu ya Azam kutoutumia uwanja wake wa nyumbani kwa mechi za Yanga na Simba. Lakini bado naunga mkono na wanaozungumzia usalama, usalama wa wawapenzi wa mpira wa miguu haulinganishwi na kitu chochote usalama ni muhimu kuliko jambo lolote. Hatuwezi kuharatarisha usalama wa mashabiki wakati hakuna miundo mbinu itakayoweza kukidhi watu elfu 40 au elfu 50.”

“Kama mazingira yanaruhusu kanuni zote zimezingatiwa kwamba uwanja unafaa kuchezewa mpira, atakaekataa atakuwa mwendawazimu, lazima mpira uchezwe Azam Coplex, Simba waende na Yanga waende hakuna namna.”

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top