CHADEMA wawalalamikia chama tawala kufanya mikutano bila kujali zuio


Hawa Mwaifunga – Makamu Mwenyekiti Baraza la wanawake Chadema na mbunge wa viti maalumu mkoa wa Tabora.

Chama cha Demokrasia na maendeleo nchini CHADEMA mkoani Tabora kimelalamikia kitendo cha baadhi ya wabunge na wanasiasa wa chama Tawala kuendelea kufanya mikutano ya kisiasa licha ya zuio lililotolewa na serikali huku jeshi la polisi likifumbia macho hatua hiyo inayodaiwa inayodaiwa kuwa ni upendeleo nje ya utawala bora.

Baadhi ya viongozi wa Chadema wamekutana hapa katika ofisi za Chama hicho wilayani Igunga ikiwa ni sehemu ya ziara ya kukiimarisha chama chao kwa kufanya mikutano ya ndani.

Kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya Siasa nchini bado inaonekana kuwa mwiba na kudai kwamba inabana Uhuru wa kuikosoa Serikali awamu ya tano kutokana na mwenendo wake tangu iingie madarakani.

Licha ya kuamini kwamba huu ni muda wa kuwatumikia wananchi kwakile walichoahidiwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, lakini Chadema imejenga imani kubwa ya kutaka uhuru zaidi wa kukutana na wananchi kwenye majukwaa ili wapate fursa ya kuelezea madhaifu ya Serikali na ikibidi kutoa ushauri katika kutatua kero zinazowakabili wananchi. 
 
 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top