VIDEO:Manchester United yaanza kwa ubabe dhidi ya Leicester Leo


Leo mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester United umepigwa kwenye dimba la Wembley ,Mechi hiyo ya kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya England imewakutanisha mabingwa
wa kombe la FA ambao ni Manchester United dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya England Leicester City. 
Manchester United wamefanikiwa kuibuka na Ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Leicester, Jesse Lingard ndiye mchezaji wa kwanza kuliona lango la Leicester Dakika ya 32 baada ya kuwatoka mabeki wa timu hiyo. Mnamo dakika ya 52 Jamie Vardy aliweza kuiwasazishia timu yake ya Leicester. 
Manchester United waliweza kufunga bao la ushindi kupitia kwa mchezaji Zlatan Ibrahimovic Dakika ya 83, Kwa matokeo hayo yamefungua ukurasa mpya wa ushindi wa kwanza wa Masheteni wekundu katika msimu huu mpya. Huu ni ushindi Mkubwa kwa kocha wa Manchester United Jose Mourinho

Video:hivi ndivyo mambo yalivyokuwa


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top