Wahamiaji haramu 71 kutoka Ethiopia wamekamatwa Leo Kigamboni DSM

Picha kutoka maktaba

Wahamiaji haramu 71 kutoka nchini Ethiopia wamekamatwa katika eneo la kigamboni jijini dsm baada ya kuingia nchini wakitokea mombasa nchini kenya kwa
njia ya bahari na baadae kusafirishwa kwa njia ya barabara kuelekea nchini afrika kusini.

Kutiwa mbaroni kwa wahamiaji hao kunatokana na taarifa za raia wema kutoa taarifa polisi baada ya kuona Lori aina ya Scania lenye namba T 246 BBG likielekea katika Ufukwe wa bahari eneo maarufu la kuingiza mali za magendo ambapo baada ya polisi kufika walifanikiwa kuwatia mbaroni dereva wa gari hilo,utingo pamoja na wakala wa wahamiaji hao haramu.

Hata hivyo baada ya kuingizwa katika gari kuelekea kituo cha polisi katika hali ya kutatanisha Mtuhumiwa namba moja aliyekuwa akiwasafirisha wahamiaji hao hakuonekana baada ya kudaiwa kushushwa njiani na askari waliomkamata hali iliyoashiria mtuhumiwa kutoa rushwa na huyu hapa dereva wa gari hilo anaeleza.

Akisimulia Mkasa huo dereva na utingo ambao ni wakazi wa mbeya walisema walikodiwa baada ya kushusha mzigo wa ndizi katika soko la ndizi manzese,na baadae wakaelezwa kuna mzigo.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top