Video&Maelezo:Tundu Lissu afikishwa mahakamani tena, Asomewa mashtaka haya



Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu saa 8. 46 huku mahakamani hapo kukiwa na ulinzi mkali.

Ulinzi uliimarishwa katika mahakama hiyo muda mrefu wakati wakimsubiria Lissu akitokea katika kituo cha polisi Kanda maalumu
.

Tundu Lissu ameshtakiwa kwa makosa matatu la kwanza kutoaa maneno ya uchochezi kwamba Agosti 2 katika Mahakama ya Kisutu kwa nia ya kujenga chuki kwa wananchi dhidi ya Rais na Serikali alitoa maneno ya uchochezi.

Shtaka la pili pia uchochezi kwamba Agosti 2 katika mahakama hiyohiyo kwa nia ya kudharau mhimili wa utoaji haki, alisema kuwa hawezi kufungwa kwa mashtaka na kesi ya upuuzi na shtaka la tatu ni la kudharau mahakama akidaiwa kuwa tarehe hiyohiyo mahakamani hapo, alitoa maneno ya uchochezi kuwa hawezi kufungwa kwa kesi na mashtaka ambayo ni upuuzi na ya kimagufulimagufuli
Tazama Video hii chini




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top