VIDEO: Koffi Olomide adaiwa kumpiga teke mwanamke Kenya

Koffi Olomide amesema hakukusudia kumpiga teke mwanamke huyo Mojawapo wa mwanamuziki mashuhuri mkongomani Koffi Olomide,amejipata matatani baada ya kunaswa kwenye kamera akimpiga teke mwanamke, anayesadikiwa kuwa mmoja wa wachezaji
ngoma wake.

Tukio hilo lilirekodiwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ambako alikuwa amewasili kwa tamasha lilopangwa kufanyika nchini Kenya. JUNIOR KHANNAAFP

Wengi wa Wakenya wamekashifu vikali kitendo hicho huku maoni katika mitandao ya kijamii yakitoa wito watu kutohudhuria tamasha hilo na badala yake wakitaka akamatwe.

Wengine kupitia kitambulisha mada #KickKoffiOlomideBackToCongo kwenye Twitter wanapendekeza afurushwe kutoka Kenya.

Kwa upande wake Koffi Olomide, kwenye ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook, amesema tukio hilo lilieleweka vibaya.
Bad news: Askari Polisi Auawa Kwa Kupigwa Risasi akiongoza magari usiku Kijitonyama Dar es Salaam bofya hapa
Amesema alikuwa anajaribu kumtetea mwanamke huyo kwani mmoja wa maafisa wa kike katika uwanja huo wa ndege alikuwa akiwasumbua wasichana hao wachezaji ngoma aliokuwa wakiandamana naye.

Katika video hiyo msichana huyo mchezaji anaonekana 
kukubaliana naye.
Tazama video hii

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top