STAA LULU KURUDI SHULE KUPIGA KOZI YA HUMAN RESOURCE


Elizabeth Micheal LULU's Profile Photo
Msanii mahiri wa filamu Elizabeth Micheal ‘Lulu’ amerudi chuoni na kuamua kuchukua kozi ya Human Resources.

Muigizaji huyo ameweka wazi anachosomea baada ya mashabiki katika mtandao wa Periscope, kutaka kujua anasomea nini baada ya kupost
video mbalimbali katika mtandao huyo huku akizungumzia maswala ya chuo.
“Jamani nimechoka kuulizwa nasomea nini, nasomea nini, nachukua Human Resources,” alisema Lulu.
Muigizaji huyo hakupenda kuweka wazi ni chuo gani anasoma, lakini aliweka wazi wiki hii naingia katika mitihani.
Lulu ni miongoni mwa wasanii wachache wa filamu walioamua kurudi darasani na kuongeza maarifa.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top