Breaking News: Wabunge wa Upinzani Waziba Midomo yao Kwa Karatasi na Plasta na Kisha Kutoka Nje ya ukumbi wa bunge

Wabunge wa Upinzani ambao wanaunda UKAWA leo Jumatatu wametoka katika Ukumbi wa Bunge kwa staili ya aina yake, Imekuwa kawaida kwa wabunge wa upinzani wanaounda Ukawa kutoka katika ukumbi
wa bunge ikiwa ni kususia vikao vinavyoongozwa na naibu spika Dk Tulia. Kitendo walichokifanya cha kuziba midomo yao kwa karatasi na utepe na kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge wakigomea kushiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika.Kitendo hicho kimewacha wabunge wa CCM na baadhi ya wapinzania ambao hawaundi Ukawa wakiwa wanawashangaa kwa kitendo cha kuziba midomo.
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema wameamua kutumia mtindo huo mpya kwa sababu Bunge limekataa kuwasikiliza hoja zao.







Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA




Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top