Mzee Kilomoni amefeli kuzuia mkutano wa Simba



Mahakama ya Wilaya ya Ilala metoa ruhusa kwa klabu ya Simba kufanya mkutano maalum wa dharura uliopangwa kufanyika December 11 mwaka huu.

Maamuzi hayo yametokana na jaribio la zuio la mkutano huo lililowasilishwa mahakamani na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo Mzee Hamis Kilomoni.

Makamu wa rais wa klabu ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amethibitisha mkutano huo utaendelea kama ulivyopangwa ambapo utafanyika kwenye bwalo la polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

“Tupo katika hatua za mwisho za maandalizi kuelekea mkutano mkuu wa dharura ambao umeitishwa na uongozi wenye ajenda kuu ya kufanya marekebisho ya katiba yetu ili hili suala la mabadiliko ya mfumo yawepo kwenye katiba na kuweza kuruhusu mtiririko wa majadiliano wa mifumo mbalimbali ili twende kwenye hayo mabadiliko ambayo tunayahitaji.”

“Leo tulipata samansi kutoka mahakama ya Ilala ikituomba tufike na kubwa ni kwamba wadhamini wetu wakiongozwa na mzee Kilomoni ndio wameenda mahakamani kuomba zuio la mkutano.”

“Tulipeleka wawakilishi wetu (wanasheria) ambao walikuwa na hoja mbalimbali, baada ya majadiliano marefu hakimu ametupilia mbali hoja za waliopeleka zuio la huo mkutano.”

Kaburu amewaomba wanachama wa Simba wawe watulivu katika kipindi hiki cha majadiliano ya mabadiliko ya mfumo ili yasije yakaharibu mwenendo wa timu katika ligi.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top