Hiki ndio Kisa cha Madrid kuwapeleka mahakamani Benfica

 eal Madrid wameripotiwa kuwapeleka mahakamani klabu ya Benfica juu ya mauzo ya mchezaji wa kiargentina Ezequiel Garay kwenda Zenit Saint Petersburg.

Madrid, ambao walimuuuza Garay kwenda Benfica mnamo mwaka 2011, walikuwa na haki ya kupata 50% ya mauzo yoyote ya mbeleni ya Garay

na wanaamini mauzo yake ya kwenda Zenit yalikuwa chini ya thamani.

Ripoti kutoka gazeti la Diario De Noticias kwamba Los Blancos wamegundua kwamba Bayern Munich walitaka kumsajili Garay akiwa Benfica, na waliweka ofa ya €15m mezani, ofa iliyokataliwa na klabu ya Ureno.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi, Garay akauzwa kwenda Zenit kwa ada ndogo ya 6 million euros.
Benfica walikuwa na haki ya kupata asilimia 40% tu ya mauzo ya mchezaji, asilimia 10 ilikuwa haki ya mmiliki wa 3 – Benfica Stars Fund.
Garay, 29, ambaye aliihama Madrid kama sehemu ya dili la Madrid kumsaini Fabio Coentrao, Garay alijiunga na Madrid akitokea Valencia kwa €20m.
Kesi hii ya Madrid vs Benfica itatolewa maamuzi baadae mwezi huu na mahakama ya michezo duniani – CAS.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top