Obama: Trump hana uwezo wa kuiongoza Marekani


Rais Obama
Rais Obama amesema kuwa kila mara Bw Trump anapoongea inabainika kwazi kwamba mgombea wa Republican hafai kuwa rais


Rais Barack Obama amemtaja Donald Trump "wa ajabu" na "asiye na ufahamu" baada ya mgombea huyo wa Republican kusema kuwa rais wa Urusi Vradimir Putin ni kiongozi mzuri zaidi kuliko Obama.

Akizungumza Laos, Bw Obama amesema kuwa kila mara Bw Trump anapoongea inabainika kwazi kwamba mgombea wa Republican hafai kuwa rais.

Katika kipindi cha televisheni siku ya Jumatano, Bw Trump alimsifu Bw Putin kuwa ni "mtu mwenye uwezo mzuri wa kudhibiti mambo" na kumpa kiwango cha asilimia 82% cha uwezo huo. 
 Donald Trump
Bw Trump alimsifu Bw Putin kuwa ni "mtu mwenye uwezo mzuri wa kudhibiti mambo" na kumpa kiwango cha asilimia 82% cha uwezo huo

Bw Trump na hasimu wake Hillary Clinton walikuwa wakijibu maswali kutoka kwa wanajeshi wa zamani.

Rais Obama alisema: "sidhani kama ana uwezo wa kuwa rais wa Marekani na kila anapozungumza, suala hili linathibitika."

Rais huyo wa Marekani alielezea kuhusu kazi ya kidiplomasia aliyokabiliana nayo katika mikutano yote wa Asean na Laos pamoja na ule wa awali wa G20 nchini Uchina.

Alisema : "Siwezi kukuelezea yote kuhusu mazungumzo niliyokuwa nayo katika kipindi cha siku nane siku tisa zilizopita na viongozi wa kigeni kwamba hii ni kazi''.

" Unapaswa kufahamu ni nini unachokizungumza, lazima kwanza ufanye kazi ya kuelewa mambo. Unapoongea , lazima kile unachokiongea kiwe kinafanana na sera unayofikiria unaweza kuitekeleza'' Alisema Obama.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top