Waziri Mkuu afanya mazungumzo na Watanzania waishio Uingereza (Picha)


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye kwa sasa yupo nchini Uingereza amekutana na Watanzania ambao wanaishi nchini humo.

Mo Blog imekuandalia habari picha pindi alipokutana na Watanzania hao.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza uliopo London wakati alipowasili ubalozini hapo kuzungumza na watanzania waishio nchini humo Mei 14, 2016. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Msafiri Marwa.




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza uliopo London kuzungumza na Watanzania Mei 14, 2016. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki , Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga na kushoto ni Jaji Mkuu wa Tamzania, Mohamed Othman.


Baadhi ya Watanzania waishio nchini Uingereza wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo London.




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania Waishio nchini Uingereza kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo London Mei 14, 2014. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga. Kushoto ni KaimuBalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Msafiri Marwa . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



SHARE.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top