AUDIO: Style ya Italia iliimaliza kabisa Simba – Kocha African Lyon





Kocha mkuu wa African Lyon Bernardo Tavares amesema waliamua kutumia style ya Italia kuimaliza Simba kwenye mchezo wa jana Jumapili na kufanikiwa kuondoka na pointi tatu mbele ya Simba ambao kabla
ya mchezo huo walikuwa hawajapoteza mechi katika michezo yao 13 tangu kuanza kwa msimu huu.

Tavares hakuacha kuipongeza Simba akisema wanatimu nzuri na wachezaji wazuri ndio maana waliweza kushinda mechi 11 na kutoka sare katika mechi mbili kati ya 13 zilizopita.

“Kwanza nianze kwa kuipongeza Simba kwasababu ni timu nzuri, kabla ya mchezo wetu walikuwa hawajapoteza mcezo hata mmoja, walishinda mechi 11 na sare mbili hakukuwa na timu iliyoifunga Simba, kwahiyo ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri.”

“Kipindi cha kwanza tulipata nafasi tatu za kufunga, mbili zikagonga ‘mtambaa panya’ wapinzani wetu pia walipata nafasi.”

“Kipindi cha pili walirudi wakiwa na mbinu ya kutumia nguvu na kutushambulia lakini tuliweza kuwadhibiti kutokana na aina ya ulinzi wa Italia tuliouweka. “ “Mbinu kwa ajili ya mchezo huu ziliwapa nafasi mabeki wangu kucheza vizuri licha ya kuwa Simba walipata nafasi japo wengine wanaweza kusema Simba walipata nafasi lakini hii ndio soka. Wakati mwingine unakuwa na bahati wakati mwingine hupati bahati, sisi tulikuwa na bahati.”

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top