Wasomi, wanaharakati wazungumzia utumbuaji

Rais John Magufuli 

Wakati tayari watumishi wengi wa umma wametumbuliwa, baadhi ya wasomi na wanaharakati wametoa mitazamo tofauti juu ya hatua hiyo kuelekea mwaka mmoja wa uongozi wa Rais John Magufuli.


Akizungumzia hatua ya Rais Magufuli kutumbua watendaji waliotumia vibaya madaraka yao, Profesa Sheriff amesema kuwajibisha watendaji siyo tatizo ila hofu yake ni namna gani taratibu na sheria zimezingatiwa.


Mwanaharakati wa masuala ya Haki za Binadamu na Haki za Kiraia wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Gema Akilimali amesema anachokifanya Rais Magufuli kinahitaji kupongezwa na kumtaka aendelee na kasi hiyo.


“Nchi ilikuwa imekosa nidhamu, watumishi walijisahau sana, walikuwa wakifanya lolote wakijua hakuna anayeweza kuwaadhibu, ukwepaji kodi ulikithiri, hivyo anawaonyesha jinsi gani alivyo makini na hilo,” amesema.


Amesema Rais Magufuli anatakiwa kuchukua tahadhari mapema badala yake atengeneze msingi wa kisheria utakaomsaidia kwa siku zijazo. 


“Anatakiwa kulishawishi Bunge litengeneze sheria zitakazomsaidia kufanya kazi ili watumishi wabakie kwenye msingi anaoutaka,” amesema.


Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wenye Ulemavu, Stella Jairos amesema Rais Magufuli yuko sahihi kwani hakuna namna nyingine ya kurejesha nidhamu ya watumishi wa umma.


Amesema kasi ya Magufuli itakuwa na manufaa makubwa kwa Watanzania wa hali ya chini kwa kuwa walikuwa wamekosa matumaini ya kunufaika na rasilimali zao na kwamba nchi ilikuwa imepoteza mwelekeo.







Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top