Msuva ametaja goli lake bora baada ya kufikisha magoli 50 Yanga



Goli la Simon Msuvu dhidi ya Mtibwa Sugar limekamilisha idadi ya magoli 50 ya kijana huyo tangu alipoanza kuichezea Yanga katika michuano yote.

Msuva alifunga bao la pili kwenye mcheo huo uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ikiwa ni mechi ya saba kwa Yanga katika ligi kuu Tanzania bara msimu huu.

Mchezaji huyo bora wa VPL 2015-2016 amesema goli analolikumbuka na ambalo ni goli bora kwake ni goli la kichwa alilofunga dhidi ya Ruvu.

Magoli 50 ya Msuva akiwa Yanga yametokana na michezo 164 katika mashindano yote tangu alipojiunga na timu hiyo ya Jangwani mwaka 2012 akitokea Moro United ya mjini Morogoro.

“Goli langu bora hadi sasa ni lile nilowafunga Ruvu mwaka juzi. Nilifunga kwa kichwa (diving header), nalifananisha na goli la Robin van Persie alilofunga kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil dhidi ya Hispania,” anaeleza Simon Msuva wakati nilipofanya nae mahojiono nikitaka kujua anapenda goli gani kati ya magoli yake 50 aliyofunga akiitumikia Yanga.

Msuvu pia hakuacha kuwashukuru watu waliopelekea mafanikio yake tangu alipojiunga na timu hiyo ya Jangwani.

“Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu, baba na mama yangu pamoja na familia nzima ya Mzee Msuva kwa kuwa bega kwa bega na mimi.”

“Pili ni kwa uongozi wa Yanga SC, makocha waliopo na waliopita katika kunitengeneza.”

“Tatu kwa wachezaji wenzangu, nne ni kwa wanafamilia wa Yanga kwa ujumla ndani na nje ya nchi kwa kuzidi kunipa support, Mwenyezi Mungu awabariki sana. Nawapenda #Goli50msuvaspeed27.”

Msuva ameshafunga magoli mawili hadi sasa kwenye ligi ligi kuu Tanzania bara timu yake ikiwa imeshacheza mechi saba.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top