Chuo Kikuu Cha DUCE chatoa neno kwa wanafunzi wake walifukuzwa kwa kumshambulia mwanafunzi


Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako 

 Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (Duce), Profesa William Anangisye amesema wangechukua hatua za kuwafukuza wanafunzi walioonekana kwenye video wakimshambulia mwanafunzi huko Mbeya


Wanachuo hao waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo, Frank Msigwa na John Deo kwa kushirikiana na Sanke Gwamaka wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere walionekana wakimshambulia Sebastian Chinguku wa Shule ya Sekondari ya Kutwa Mbeya.


Profesa Anangisye amesema kitendo walichokifanya ni cha kinyama na kimekiuka maadili ya ualimu na kwamba kwa mujibu wa taratibu za taaluma hiyo, mwalimu mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kumuadhibu mwanafunzi.


“Tunalaani kitendo walichokifanya wanafunzi wetu kimetutia aibu. Hata kama Serikali isingechukua hatua, uongozi wa Duce tusingeweza kuvumilia unyama huo. Tungewatoa maana tayari wamekiuka miiko ilhali tulikuwa tukiwaandaa kuwa walimu,” amesema.


Baada ya tukio hilo kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya habari, Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako alitangaza kuwatimua chuoni akisema kitendo hicho ni kosa la jinai.


Hata hivyo, wiki mbili zilizopita, wahadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa, Dk Hellen Myeya na Anneth Kasebele waliwakagua wanafunzi hao lakini hawakupata malalamiko yoyote wala kugusiwa kama kuna tatizo.







Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top