Maazimio 8 ya UKAWA kukabiliana na Prof. Lipumba na Msajili wa vyama


Umoja wa Katiba ya Wananchi umedhamiria kwenda mahakamani kumshtaki Prof. Lipumba na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutokana na mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF).



Katika kikao walichofanya jana, UKAWA walipitisha maazimio kukabiliana na mgogoro unaoendelea ndani ya CUF. Maazimio hayo ni pamoja na;-
Hatumtambui Prof. Lipumba kama mwanachama wa CUF na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA
UKAWA wanautambua uongozi wa Julius Mtatiro na Maalim Seif
Wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA wasitoe ushirikiano kwa Prof. Lipumba na washirika wake
Wenyeviti wa mitaa, vijiji, Madiwani, Wabunge wasitoe ushirikiano kwa Prof. Lipumba na washirika wake
Wabunge wote wanaomuunga mkono Prof. Lipumba watatimuliwa ndani ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
Ushirikiano wa kisiasa Tanganyika na Zanzibar utashughulikiwa na UKAWA
Mawakili wa UKAWA watamfunguliwa mashtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwa matumizi mabaya ya madaraka na
Mawakili wa UKAWA watamfungulia mashtaka Prof. Lipumba.

Kwa upande wake Prof. Lipumba aliwataka wanachama wa CUF kuwa wamoja na kusema kuwa yeye hajali kuhusu UKAWA kikubwa anachoangala ni kuijenga upya CUF.
 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top