Kila kukicha mgogoro ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) unazidi kuchukua sura mpya. Jana viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi wamekutana kujadili mgogoro wa CUF sababu ni moja ya vyama vinavyounda UKAWA.
Viongozi wa UKAWA jana wametangaza kuwa hawamtambui Prof. Lipumba kama mwenyekiti wa CUF na kuwa wao watashirikiana na viongozi halali wa CUF, na kutilia maanani maazimio yaliy0pitishwa katika vikao halali vya CUF.
Aidha, mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amewataka viongozi wa chama hicho nchini kote kumpuuza na kutompa ushirikiano Prof. Lipumba kwani ni msaliti.
Kwa upande wake yeye, Prof. Lipumba ameendelea kutekekelza majukumu yake kama Mwenyekiti wa CUF ambapo jana ametangaza kutengua uteuzi wa Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za Chama cha Wananchi (CUF).
Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa ni pamoja na;-
Joran Bashange – Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha
Ismail Jussa- Mkurugenzi wa Mambo ya Nje
Mustafa Wandwi- Mkurugenzi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
Kurufumu Mchuchuli- Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria
Shaweji Mketo- Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi na
Abdalla Mtolea- Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje
Aidha Prof. Lipumba amesema kuwa hajali kama viongozi wa UKAWA wanamtaka au hawamtaki kwani yeye anachojali ni kuijenga CUF.
Mpina ataka wanaosoma 'cheti' nao wapewe mikopo bofya hapa
Pato La Taifa Lakua Kwa Asilimia 7.9 bofya hapa
Maalim Seif 'Kumshitaki' Lipumba kwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) bofya hapa
UPDATED!: List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017 bofya hapa
Manispaa ya Temeke kugawanywa bofya hapa
Mapokezi ya viongozi CUF yaota mbawa bofya hapa
Wachambuzi wa uchumi watoa neno kwa ATCL bofya hapa
Wawakilishi wapitisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar bofya hapa
Simba, Yanga mwendo wa kimya kimya bofya hapa
Korti yatupa kesi dhidi ya Pierre Nkurunziza bofya hapa

Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)