Audio: Serikali yapiga marufuku Simba, Yanga, kutumia uwanja wa taifa




Waziri mwenye dhamana ya michezo Mh. Nape Nnauye amepiga mafuruku vilabu vya Simba na Yanga kuutumia uwanja wa taifa kwa muda usiojulikana kutokana na uharibifu wa miundombinu ya uwanja
huo wakati wa mechi ya Jumamosi October 1.

Mechi ya jana iliacha hasara ya kung’olewa kwa viti vya uwanjani na kutupwa uwanjani vikitumiwa kama silaha lakini pia mageti manne yalivunjwa.



Kaimu Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Alex Nkenyenge amethibitisha uharibifu ulianzia nje ya uwanja ambapo mageti manne yaling’olewa na mashabiki wa mchezo wa jana wakilazimisha kuingia bila kufata utaratibu.

Kwa upande wa ndani viti 1781 viling’olewa kutoka upande ambao walikuwa wamekaa mashabiki wa klabu ya Simba.



Kila kiti kimoja kinathamani ya shilingi 220,000 kwahiyo kwa hesabu za haraka, thamani ya viti vilivyong’olewa ni zaidi ya shilingi milioni 300 za Tanzania.

Waziri Nnauye akatoa kauli ya serikali kwa yote yaliyotokea kwenye mchezo wa Yanga vs Simba ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku vilabu hivyo kutumia uwanja wa taifa.



“Nadhani jambo hili linaendelea kwasababu tumekuwa tukitoa adhabu kwa vilabu kwahiyo mashabiki hawaoni kama wana wajibu wa kuhakikisha wanatunza mali hizi wakijua vilabu vitalipa.”

“Lakini nadhani tuchukue hatua kubwa zaidi ya hapa, kuanzia sasa uwanja huu hautatumika kwa Yanga na Simba mpaka tutakapoamua baadaye, watafute viwanja vingine.” Msikilize Mh. Nnauye akipiga marufuku Simba na Yanga kuutumia uwanja wa taifa. 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top