Trump: Aliyeiga hotuba ya Obama akiri kosa





Mke wa Trump adaiwa kumuiga Michelle Obama

Mfanyakazi mmoja wa bwenyenye mgombea kiti cha urais wa Marekani kwa tikiti cha chama cha Republican Donald Trump, amekiri kuiga hotuba ya Bi Michelle Obama alipokuwa akiandika hotuba hiyo
iliyosomwa na Melania.

Meredith McIver amekiri kuwa ndiye aliyemsaidia mkewe Trump, Melania katika uandishi wa hotuba hiyo iliyovutia hisia kali kwenye mitandao ya kijamii kote duniani huku wengi wakimkosoa kwa kuiga dhana ya bi Obama.
Donald Trump kugombea urais Marekani

McIver amesema kuwa alikiri makosa yake na akaomba ruhusa ajiuzulu lakini ombi lake limekataliwa.

Mke wa Trump adaiwa kumuiga Michelle Obama Donald Trump kugombea urais Marekani
Sherehe ya ufunguzi wa kongamano kuu la wajumbe wa chama cha Republican nchini Marekani iligubikwa na utata hapo jana baada ya hotuba iliyotolewa na mke wa Donald Trump Melani kufanana na ile ya ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle, aliyoitoa miaka minane iliyopita.

Mke huyo wa Trump, ambaye ni mzaliwa wa Slovenia, amekiri kuwa alipata usaidizi mdogo katika uandishi wa hotuba hiyo.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top