Audio: Simba ni zaidi ya Yanga – Mayanja




Jackson Mayanja ametamba kwamba kikosi chao kipo sawa ndio maana wachezaji waliweza kupambana kupata bao na hatimaye kuvuna pointi moja licha ya kucheza pungufu kwa muda mrefu huku wakiwa nyuma
kwa goli 1-0 mbele ya Yanga.

Kocha huyo wa zamani wa Kagera Sugar na Coastal Union amesema, wachezaji wameonesha umoja na kujituma kama timu hatimaye kupata matokeo.

“Licha ya kuwa pungu kwa mchezaji mmoja tuliweza kupata goli la kusawazisha, hiyo imeonesha umoja na kujituma kwa timu. Siwezi kuongea vitu vingi lakini ilikuwa ni vizuri kwetu kupata hiyo pointi moja”, amesema Mayanja mara baada ya mechi kumalizika.

“Inawezekana huu ni mwaka wetu pia kwasababu bado tunawachezaji ambao wako fresh kuliko timu ya Yanga ndiyo maana waliweza kucheza dhidi ya wachezaji 11 wa Yanga, hiyo inaonesha jinsi gani tuko fit.”

Mayanja amesema hatawezi kuiongelea kadi nyekundu aliyopewa Jonas Mkude wala mwamuzi wa mchezo, kwasababu haikubadili chochote.

“Siwezi kuzungumzia kadi nyekundu wala mwamuzi lakini haijapunguza kitu chochote kwasababu tuliweza kupata goli la kusawazisha na tulikuwa na nafasi ya kushinda mechi dakika za mwisho kama tungeendelea kushambulia.”

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top