Audio: Msimu huu hakuna wa kutuzuia – Manara




Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema msimu huu hakuna wa kuizuia Simba kuanzia TFF, marefa na mtu yeyote yule
.

Manara anamshutumu mwamuzi wa mchezo wao dhidi ya Yanga Martin Saanya kwa kuipendelea Yanga kwasababu mfungaji wa goli la Yanga (Amis Tambwe) aliushika mpira kabla hajafunga.

“Hii ni ishara kwamba hatutazuilika na TFF, referees na mtu yeyote, mwaka huu ni wetu hakuna mtu wa kutuzuia, tunao uwezo timu yetu tumeiona”, amesema Manara ambaye alionekana wazi kuwa na jazba.

“Tunaenda kuangalia marudio, tukiona kwa namna yeyote ile Yanga walibebwa hatutakubali, safari hii kuna jambo litatokea zaidi ya mpira, haiwezekani timu moja ikawa inabebwa kwa mbeleko ya chuma, Jumatatu nitazungumza na waandishi wa habari.”

“Klabu ikiona kitu cha tofauti, itachukua hatua za makusudi. Kwasababu timu hii inabebwa, ikienda kwenye mashindano ya Caf raundi ya kwanza nje.”

“Hatuungi mkono vurugu, lakini mechi hii ina-tension kubwa lazima marefa wajitahidi kuchezesha kwa haki, hakuna asiyeona kwamba yule mchezaji aliushika mpira. Hatutaki fujo unalazimisha watu wafanye fujo.” Msikilize Haji Manara hapa chini anavyotamba kwamba msimu huu hakuna wa kuizuia Simba 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top