Tweet ya Zitto Kabwe juu ya goli la Tambwe vs Simba




Mechi za Simba na Yanga zina raha yake, achana na mchezo wenyewe unaopigwa uwanjani ndani ya dakika 90 bali hata nje ya uwanja huwa kuna mambo ambayo yanaleta burudani hasa mashabiki wa timu hizi mbili
kongwe Tanzania.

Baada ya mchezo wa October 1 kumalizika kwa sare ya Yanga 1-1 Simba, kumekuwa na mjadala mkubwa unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu goli la Yanga lililofungwa na Amis Tambwe hatimaye kupelekea nahodha wa Simba Jonas Mkude kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na kumzonga mwamuzi kwa kulikubali goli hilo linalodawa kuwa, Tambwe aliushika mpira kabla ya kuutumbukiza kambani.

Munge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe ali-tweet kwenye account yake ya twitter ujumbe wa kuibeza Yanga kutokana na goli hilo, ujumbe unasomeka: “Mkono wa Tambwe washindwa kuibeba Yanga.”



Zitto ni shabiki mkubwa wa Simba na mara kadhaa timu yake inapocheza amekuwa aki-tweet jumbe mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kuhusu timu yake.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top