TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TCU JUU YA UJUMBE UNAOSAMBAA KUHUSU KUTANGAZWA KWA ORODHA YA WANAFUNZI WALIODAHILIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

tcu banner
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kuuarifu umma kwamba, kuna taarifa za uongo ambazo zimesambazwa na mtu/watu wasio waadilifu kuwa hivi punde majina ya wanafunzi waliodahiliwa kujiunga katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu hapa nchini kwa mwaka wa masomo 2016/2017 yatatanganzwa. 

Aidha, taarifa hiyo inawataka watu wanaohitaji msaada wa haraka zaidi kujua chuo alichochaguliwa walipe Tshs. 1,000/= (Shilingi Elfu Moja) kwa njia ya simu.

TCU inapenda kukanusha kuwa taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote, hivyo zipuuzwe. Huu ni utapeli, hivyo tunawatadharisha wale wote walioomba kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini kuwa makini na kuhakikisha kuwa wanawasiliana na TCU ili kupata taarifa sahihi. 

TCU inalaani kitendo hicho cha kuchapisha na kutangaza taarifa za uongo na hivyo kusababisha mkanganyiko katika jamii. Kitendo hiki ni uvunjifu wa sheria za nchi, na kamwe hakiwezi kuvumiliwa 
kwa misingi yoyote ile. Kwa sababu hiyo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote aliyehusika na uchapishaji na usambazaji wa taarifa hizi za uongo. Tunapenda kuukumbusha umma, vyuo vikuu na wadau wote wa elimu ya juu hapa nchini kwamba taarifa rasmi za TCU hutolewa na Katibu Mtendaji au Mwenyekiti wa Tume na huwekwa ama kwenye tovuti ya TCU ambayo ni www.tcu.go.tz au kwenye magazeti. Imetolewa na Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 30 Agosti, 2016
Taarifa zaidi tembelea http://www.tcu.go.tz/



Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top