GENK YAITAHADHARISHA TFF JUU YA SAMATTA


Klabu ya Genk ambayo anacheza nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta, imetoa tahadhari kwa benchi la ufundi la Taifa Stars hasa hususan upande wa madaktari juu ya Mbwana Samatta ambaye ataungana na kikosi cha Mkwasa moja kwa moja Lagos, Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika nchini Gabon mwaka 2017.

Afisa habari wa TFF amethibitisha tahadhari hiyo waliyopewa juu ya usalama wa Samatta katika mchezo huo.

“Kauli hii imekwenda sambamba na hali ya uchezaji wa mchezaji mwenyewe, ambapo katika maelekezo wamesema wanaheshimu timu za taifa " Alisema Afisa habari TFF

“Genk wameshauri kwamba, kabla ya Samatta ahajacheza ni vizuri akapimwa kwanza kwasababu alipewa majukumu mazito ambapo alipewa mazoezi magumu ya kuwa fit ili kuhakikisha anaisaidia timu yake kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Europa League. Kwahiyo walitaka kuona anapata muda wa kupumzika lakini imebidi wamwachie kwasababu anahitajika kwenye timu ya taifa.”

Tanzania dhidi ya Nigeria Zitamenyanya katika mchezo wa kukamilisha ratiba ambapo Misri wameshafuzu kutoka katika Kundi hilo la G.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top