News alert:David Luiz arudi Chelsea

Chelsea wamekamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Brazil David Luiz kutoka Paris Saint-Germain kwa ada ya paundi mil 38 (euro mil 45).

Luiz (29) anarejea Chelsea baada ya kuondoka klabuni hapo miaka miwili iliyopita baada ya kusajiliwa ba PSG kwa ada ya paundi mil 50.

Inaarifiwa kuwa tayari Luiz amefuzu vipimo vya afya na kusaini mkataba ambao hata hivyo bado haujawekwa wazi.

PSG bado hawajasajili mbadala wa Luiz kutokana kuwa tayari na mabeki watatu wanaoweza kucheza katikati ambao ni Thiago Silva, Marquinhos na Presnel Kimpembe, huku Serge Aurier ambaye anacheza beki ya kulia akiwa pia na uwezo wa kufanya hivyo pia.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top