VIDEO- BEKI APEWA KADI NYEKUNDU BAADA YA KUFUNGA HAT-TRICK SWEDEN

Huko nchini Sweden kunako Ligi Kuu ya nchini humo, beki wa kati wa Norrby IF Medi Dresevic alifunga hat-trick katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Tvaaker na kutolea kwa kadi nyekundu
.


Hilo lilikuwa tukio kubwa mno kwa beki huyo, kwani katika maisha yake ya soka rasmi la ushindani amewahi kufunga goli moja tu mwaka 2011 wakati timu yake iliposhinda mabao 3-2 dhidi ya Rosengård.

Medi Dresevic alishangilia goli lake lililokamilisha hat-trick kwa kukimbilia kwenye viti vya mashabiki na kukaa kwa muda huku akijipongeza kwa kujipigia makofi.

Baada ya tukio hilo, kutokana na hapo awali kuwa na kadi ya njano, mwamuzi alimzawadia kadi nyekundu huku wachezaji wenzake pia wakimlalamikia vibaya kwa kitendo chake kilichopelekea adhabu hiyo.

Adhabu hiyo itapelekea mchezaji huyo kukosa mchezo wao muhimu unaofuata.

Angalia video
 Medi firar sitt hattrick med att gå upp på läktaren för att applådera sig själv. Glömde av sitt gula #ettanfotboll pic.twitter.com/qi0DJBZXDr

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top