Majina ya wakurugenzi wa halmashauri 13 ‘waliokacha’ uteuzi wa JPM


Katika uteuzi ulifanywa mwezi Julai na Rais Magufuli wa wakurugenzi wa Halmashauri mbali mbali za miji na wilaya, ambao ulitangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe, kati ya wakurugenzi
wote 185 walioteuliwa, 65 waliteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 walikua wakurugenzi wapya kabisa. Kati yao Wakurugenzi 13 hawakuripoti kabisa katika vitengo vyao vya kazi kwa sababu tofauti tofauti kama kuwepo masomoni, kupatwa na ugonjwa au hali ya kiafya kutokumruhusu kushika wadhifa wowote na wengine kutokua na sifa za kitaaluma hivyo kushindwa kukidhi vigezo vya kuendelea kuwepo kwenye nafasi hizo.

Licha ya Serikali kushindwa kuyataja majina ya Wakurugenzi ambao hawakuripoti katika vituo vyao vya kazi au kutoa sababu za wao kushindwa kuripoti kazini, Tumeweza kufanya uchunguzi na kugundua Wakurugenzi waliteuliwa mwezi Julai ambao hawatashika nyazifa hizo kutokana na Rais kuteua Wakurugenzi wengine kushika wadhifa huo siku ya tarehe 10 mwezi Septemba.

Majina ya wakurugenzi 13 ambao hawatashika nafasi zao hizo kutokana na sababu zisizojulikana:

Bagamoyo DC – Azimina A. Mbilinyi

Mkalama DC – Martin Msuha Mtanda

Karatu DC – Banda Kamwande Sonoko

Moshi DC – Emalieza Sekwao Chilemeji

Kibondo DC – Shelembi Felician Manolo

Nachingwea DC – Bakari Mohamed Bakari

Ulanga DC – Audax Christian Rukonge

Nsimbo DC – Joachim Jimmy Nchunda

Mbulu DC – Festi Fungameza Fwema

Ukerewe DC – Tumaini Sekwa Shija

Bukoba DC – Abdulaaziz Jaad Hussein

Tarime Mji – Hidaya Adam Usanga

Dodoma Manispaa – Dkt. Leonard M. Masale

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima, Toleo namba 4304, Septemba 15,2016

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top