TV1 kuonyesha Ligi Kuu ya England



 Mashabiki wa soka nchini wamepata ahueni ya kutazama Ligi Kuu ya England kupitia kituo cha runinga cha TV1.


Meneja Mkuu wa TV1, Joseph Sayi amesema kituo chao kimepata ruhusa kutoka kampuni
ya Econet Media yenye haki za kuonyesha ligi hiyo kusini mwa Jangwa la Sahara.


“Kama inavyofahamika kuwa Ligi Kuu England inatazamwa na watu zaidi ya milioni 260 duniani, hivyo tumeona tuwafikishie uhondo huu mashabiki wa soka nchini kwa urahisi,” amesema Sayi.


Meneja Masoko wa TV1, Gillian Lugumamu amesema kituo hicho kitaonyesha mechi moja kila Jumamosi, huku Ijumaa na Jumatano zikitengwa kwa ajili ya uchambuzi wa mechi za ligi hiyo.
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi August 04, 2016 bofya hapa


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top