Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi hajaripoti kwenye kituo chake cha kazi


Rais John Magufuli

 Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Emalieza Chilemeji hajaripoti kwenye kituo chake cha kazi
.Chilemeji ni miongoni mwa wakurugenzi 120 wapya walioteuliwa na Rais John Magufuli Julai 7.


Chanzo kutoka ndani ya Halmashauri hiyo kililidokeza kuwa mkurugenzi aliyeondolewa Moshi, Fulgence Mponji alikuwa ameshaandaa hati ya makabidhiano lakini ameshindwa kukabidhi ofisi kutokana na mrithi wake kutotokea.


Mponji amethibitisha kuwa mrithi wake hajaripoti kazini lakini akasema hajui sababu za kutoripoti hadi sasa na wala hajui yuko wapi na kutaka asiulizwe suala hilo.


“Ilibidi (Mponji) aendelee kuchapa kazi siku zote hizo karibu 20 hadi juzi juzi hivi alipoamua kwenda zake likizo. Hatujui amekataa uteuzi au yuko wapi maana si kawaida,” amedokeza mtumishi mmoja.





Julai 7, Rais Magufuli alitangaza kuteua wakurugenzi 185 wa halmashauri za miji, majiji na Manispaa na kati yao, wakurugenzi 120 ni wapya.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top