Marufuku ‘Ukuta’ Mbeya



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla 

 Mikutano ya Operesheni Ukuta iliyotangazwa kuratibiwa na Chadema kuanzia Septemba Mosi, imepigwa marufuku na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
, Amos Makalla.


Akizungumza katika kikao cha kazi kilichoshirikisha kamati ya ulinzi na usalama mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri, Makalla ametangaza kupiga marufuku mkutano wowote utakaofanyika chini ya utaratibu unaoitwa Operesheni Ukuta.


“Bila shaka wananchi Mbeya wanataka amani na kazi, hivyo ni marufuku kufanyika mkutano wowote wa kisiasa unaoandaliwa kwa kushirikiana na watu wengine kutoka nje ya mkoa,” amesema Makalla aliyewahi kuwa mbunge na mweka hazina wa CCM.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top