Bavicha yaunga mkono "UKUTA"


Mwenyekiti wa Bavicha Taifa,Patrobas Katambi akizumngumza jijini Dar es Salaam  kuhusu msimamo wao wa kuendesha operesheni Ukuta. Kulia ni Katibu Mkuu wa Bavicha Taifa, Julius Mwita .Picha na Omar Fungo

Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) limetangaza kuunga mkono azimio la Kamati Kuu la kufanya mikutano nchi nzima kuanzia Septemba mosi, mwaka huu.


Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi amesema watafuata taratibu zote za kisheria ikiwamo kutoa taarifa na kuomba ulinzi wa polisi.


Katambi amesema ajenda za mikutano hiyo zitakuwa ni kupinga ukandamizaji wa demokrasia nchini, pamoja na kupinga hatua ya viongozi wa vyama vya siasa kukamatwa na polisi mara kwa mara bila sababu za msingi.


"Wote tunaona jinsi Serikali inavyoingilia mihimili mingine. Mahakama ndiyo chombo pekee ambacho kinatoa haki, kama mhimili huu unaingiliwa basi hata hukumu zinazofanyika zitakuwa za mashaka," amesema Katambi.


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top