YANGA YAMUONGEZA KANDARASI YA MIAKA MIWILI HANS PLUIJM

Kocha Hans van der Pluijm amesaini kandarasi ya miaka miwili kuendelea kuitumikia timu ya soka ya Yanga.

Pluijim amekua na mafanikio makubwa kwa timu ya Yanga baada ya kuiwezesha timu hiyo msimu huu kunyakua makombe mawili,moja likiwa ni la ligi kuu ya Tanzania bara na la pili ni la FA

Aidha amefanikiwa kuipeleka timu hiyo katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika ambapo kwa sasa kikosi cha timu hiyo kinaendelea na maandalizi ya michuano hiyo.

Msimu wa mwaka 2014-205 Puluijim aliiwezesha Yanga kubeba taji la ligi kuu ya Tanzania bara huku wakiwa na mechi mbili mkononi hivyo ni jambo jema kwa Yanga kuendelea kua nae kocha huyo kutoka Uholanzi anayelifahamu vizuri soka la Afrika.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top