Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya mikopo elimu ya juu, Jerry Sabi
Wanafunzi 2,739 mbalimbali hawakujitokeza kuhakikiwa wakati Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilipofanya shughuli hiyo katika vyuo 26 nchini
.
.
Kaimu Mkurugenzi wa bodi hiyo, Jerry Sabi amesema taarifa hiyo ni ya awali baada ya uchambuzi taarifa za uhakiki wa vyuo 18 kati ya 26 vilivyohakikiwa.
Amesema bodi hiyo imetoa siku saba kuanzia leo kwa wanafunzi ambao hawajahakikiwa kujitokeza ili wahakikiwe vinginevyo wataonekana kuwa ni wanafunzi hewa.
Amesema Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ndicho kinachoongoza kuwa na wanafunzi wengi wasiohakikiwa wanaofikia 763.
"Tunatoa muda wa ziada ili wanafunzi ambao hawakupata nafasi ya kuhakikiwa kufanya hivyo vinginevyo tutafuta mikopo yao," amesema.
Amesema orodha ya wanafunzi wasiohakikiwa iko kwenye anuani ya mtandao wa bodi hiyo ambayo ni www.heslb.go.tz.
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatano July 13, 2016 Bofya hapa
Wafuasi wa Steven Wassira wambwaga Ester Bulaya Bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)