Bi Mossi Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi
Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.
Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.
Bi Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali
ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.
ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.
Mbunge huyo aliwahi kufanya kazi na idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Msemaji wa rais wa Burundi Bw Willy Nyamitwe amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.
“Nimesikitishwa sana. Dadangu mkubwa Hafsa Mossi, mwanachama wa @EA_Bunge amefariki, amepigwa risasi na wahalifu. R.I.P #Burundi,” ameandika kwenye Twitter.
Waziri wa mambo ya nje Alain Aime Nyamitwe pia ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo.
“Nimehuzunishwa sana na mauaji ya leo#Bujumburaya Mheshimiwa Hafsa Mossi, na mwanachama wa#EALA. Ni hasara kuu kwa taifa na#EAC,” ameandika kwenye Twitter.
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatano July 13, 2016 Bofya hapa
Wafuasi wa Steven Wassira wambwaga Ester Bulaya Bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)