Tetesi za soka Ulaya Jumatano 13.07.2016

Beki wa England John Stones, 22, ameiambia klabu yake ya Everton kuwa anataka kujiunga na Manchester City (Liverpool Echo).
StonesImage copyrightGETTY
Image captionJohn Stones anafuatiliwa na Man City
Mshambuliaji Wilfried Bony, 27, anajiandaa kuondoka Manchester City, huku Galatasaray wakitoa pauni milioni 3 za kumsajili kwa mkopo (Sun), Leroy Sane, 20 anayesakwa na Manchester City
, hajaiambia klabu yake ya Schalke kuwa anataka kuondoka, wakati meneja mpya wa City Pep Guardiola akiwa tayari kutoa pauni milioni 40 kumsajili kiungo huyo Mjerumani (Daily Star).
FabregasImage copyrightGETTY
Image captionFabregas kuungana tena na Mourinho?
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kumsajili kiungo kutoka Spain, Cesc Fabregas, 29, ambaye alikuwa naye Chelsea (Daily Mirror), Mourinho huenda akaamua kumfuatilia kiungo wa Newcastle, Moussa Sissoko, 26, iwapo atashindwa kumsajili Paul Pogba kutoka Juventus (Le 10 Sport), Man United wanaendelea kumfuatilia beki wa West Ham, Reece Oxford, 17 (Evening Standard), meneja msaidizi wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs, 41, atacheza katika ligi kuu ya India mwezi huu (Daily Mail).
GiroudImage copyrightPA
Image captionWenger anataka kumuondoa Giroud
Meneja wa Sunderland Sam Allardyce anaonekana huenda akatajwa kuwa meneja wa England na Gary Neville kuwa msaidizi wake (Daily Mirror), dau la pauni milioni 25 la Arsenal kumtaka beki Daniele Rugani, 21, limekataliwa na Juventus (Calciomercato), Arsenal wako tayari kuwapa Napoli Olivier Giroud, 29, pamoja na pauni milioni 42, ili wamsajili Gonzalo Higuain, 28 (Sun), Arsenal na Chelsea wanamfuatilia beki wa Roma Kostas Manolas, 25 (Corriere Dello Sport).
MorataImage copyrightREUTERS
Image captionChelsea wanamnyatia Morata
Chelsea wana wasiwasi kuwa huenda wakalazimika kulipa zaidi ya pauni milioni 50 kumsajili beki Kalidou Koulibaly, 25, kutoka Napoli (Evening Standard), Real Madrid wameingia kwenye mbio za kumsajili kiungo wa Valencia Andre Gomes anayefuatiliwa na Chelsea (Fichajes), Madrid wameamua kutomuuza mshambuliaji wao, Alvaro Morata, 23, kwenda Chelsea (Daily Mail).
NegredoImage copyrightPA
Image captionNegredo kurejea tena England?
Liverpool na Tottenham hawajakatishwa tamaa na bei ya pauni milioni 25 iliyowekwa kwa beki wa Kols, Jonas Hectors, 26 (Bild), Middlesbrough waliopanda daraja wanataka kumsajili beki wa Chelsea Tomas Kalas, 23 (Daily Express), Middlebrough pia wana matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Valencia Alvaro Negredo, 30, aliyeichezea Manchester City kwa misimu miwili (Guardian).
Henry aondoka Arsenal hii ndio sababu bofya hapa
KanuImage copyrightAFP
Image captionRobson Kanu alionesha cheche zake Euro 2016
Swansea wanataka kupanda dau kumsajili Leonardo Ulloa, 29, kutoka Leicester, wakati wakijiandaa kwa kuondoka kwa Andre Ayew na Bafetimbi Gomis (Daily Telegraph), mshambuliaji wa Wales Hal Robson-Kanu ambaye ni mchezaji huru amepewa mshahara wa pauni 100,000 kujiunga na Ligi Kuu ya China (Daily Mirror).
SissokoImage copyrightAFP
Image captionBei ya Moussa Sissoko inaogopesha watu
Wawakilishi wa Moussa Sissoko wamemtaka meneja wa Newcastle, Rfael Benitez, kuingilia kati mzozo kuhusu bei ya pauni milioni 35 aliyowekewa kiungo huyo ambayo wanahisi inamzuia kuondoka (Daily Mirror), Newcastle wako tayari kusikiliza dau la kuanzia pauni milioni 20 kumsajili Sissoko, 26, ambaye aling’ara kwenye michuano ya Euro 2016 (Times), Marseille wataelekeza nguvu zao kumtaka Carlos Sanchez, 30, baada ya kushindwa kumpata Idrissa Gana kutoka Aston Villa (Birmingham Mail).


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top