Henry aondoka Arsenal

Henry hakutaka kuacha kazi ya uchambuzi wa soka


Thierry Henry ameondoka Arsenal, baada ya kukataa nafasi aliyopewa ya kufundisha wachezaji wa chini ya umri wa
miaka 18.

Henry, 38, alipewa nafasi hiyo na meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ambaye alimuambia kuwa hawezi kuchanganya na kazi yake ya sasa kama mchambuzi wa soka kwenye TV.

Hata hivyo, Henry ambaye alifanya kazi na wachezaji chipukizi wa Arsenal kama sehemu ya mafunzo ya kupata leseni yake ya ukocha ya Uefa, hakuwa tayari kuacha kazi yake ya uchambuzi wa soka.

Nahodha wa zamani wa Arsenal, Tony Adams, 49, sasa atachukua nafasi hiyo ya vijana chini ya miaka 18.
Henry sasa lazima atafute timu ya kufundisha ili kukamilisha leseni yake ya ukocha.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top