Mwenyekiti
wa TLP taifa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema amesisistiza ombi lake la
kazi kwa kumkumbusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kwamba ampe kazi yoyote
amsaidie kibarua kigumu alichonacho cha kuwahudumia wananchi
amsaidie kibarua kigumu alichonacho cha kuwahudumia wananchi
Dkt.
Mrema ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu miaka 32
ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Moringe Sokoine
ambaye alihudumu kwenye awamu ya kwanza ya Mwl. Julius Nyerere ambapo
alifariki akiwa na cheo cha waziri mkuu tarehe 12.04.1984 kwa ajali ya
gari.
''Namkumbuka
Sokoine kama mtu wa watu aliyehudumia watu,aliyepambana na ufisadi na
magendo .Alikuwa anatenda haki kwa wananchi wote .
"Hata
mimi nilipokuwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu
nilijaribu kufanya kama yeye bahati mbaya sikufanikiwa kama yeye kwa
sababu sikuwa waziri mkuu au Rais''- Alisisistiza Mrema.
Kuhusu Mrema kuomba kazi kwa Dkt. Magufuli
Mrema
alisema kwa kutambua rekodi yake ya utendaji kazi wa Rais Dkt.
Magufuli, aliwahimiza wananchi wa Vunjo wamchague kipindi cha kampeni na
yeye akampigia kampeni na Rais akawaambia wananchi wa Vunjo kwamba
Mrema akikosa ubunge atapangiwa kazi nyingine ndiyo hiyo wananchi
wanaulizia.
Aidha Mrema alisema kuna maeneo ambayo yeye anafiti siyo lazima apewe madaraka makubwa
"Mimi
sihitaji ukuu wa mkoa au uwaziri, anipe kazi yoyote na nikionana naye
nitamkonyeza maeneo ambayo ninafiti ili nimsaidie kutumbua majipu."
Alisema Mrema
Hata
hivyo Dkt. Mrema alimpongeza Dkt. Magufuli kwamba ni mtendaji ambaye
ameamua bila kusukumwa kupambana na mafisadi na kwamba yeye ni alfa na
omega na kazi hiyo ameonyesha kwamba atafanya vizuri kuliko Sokoine na
Mrema.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)