Rashford atajwa kikosi cha Uingereza cha Euro

Rashford ana umri wa miaka 18

Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amemtaja chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford kwenye kikosi chake cha <Endelea bofya kichwa cha habari hii juu>wachezaji watakaocheza Euro 2016.

Rashford, 18, alianza kuchezea timu kuu ya Uinted kipindi cha pili cha msimu lakini aliwika mara moja.

Alifunga mabao manne mechi zake mbili za kwanza na aliwafungia mabao saba katika mechi 16 tangu aanze kuwachezea 25 Februari.

Hodgson ametaja kikosi cha wachezaji 26, ambacho kitapunguzwa baadaye hadi wachezaji 23.

Winga wa Newcastle United Andros Townsend na kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere pia wamo kwenye kikosi hicho kitakachopigania ubingwa Ufaransa, kwenye michuano hiyo itakayoanza tarehe 10 Juni.

Lakini nyota wa Arsenal Theo Walcott, Phil Jagielka (Everton) na Mark Noble wa West Ham hawamo kikosini.

Siku ya mwisho kwa mataifa 24 yanayoshiriki kutangaza timu zao za wachezaji 23 ni tarehe 31 Mei.
Kikosi

Walinda lango: Joe Hart (Manchester City), Fraser Forster (Southampton), Tom Heaton (Burnley).

Mabeki: Gary Cahill (Chelsea), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur), Ryan Bertrand (Southampton), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Nathaniel Clyne (Liverpool).

Viungo wa kati: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Fabian Delph (Manchester City), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Danny Drinkwater (Leicester City), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Andros Townsend (Newcastle United), Jack Wilshere (Arsenal).

Washambuliaji: Wayne Rooney (Manchester United), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Jamie Vardy (Leicester City), Daniel Sturridge (Liverpool), Marcus Rashford (Manchester United).

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top