MAYANJA ATIA DOLEGUMBA SIMBA


mayanja

Jackson Mayanja amesaini mkataba wa kuwa kocha msaidizi wa Joseph Omog katika klabu ya Simba.

Mayanja alipewa mkataba mfupi
kuwa kocha msaidizi kwenye klabu hiyo ya Msimbazi chini ya Dylan Kerr baada ya Selemani Matola ambaye alijiuzulu na kuelekea Geita Gold Sports.

Awali kulikuwepo kwamba klabu yake ya Kagera Sugar ilikuwa ikitaka kumrejesha kocha huyo raia wa Uganda lakini kocha huyo aliamua kubakia Msimbazi.

Mayanja aliiongoza Simba kwenye mzunguko wa pili wa VPL baada ya timu hiyo kumtimu aliyekuwa kocha mkuu Dylan Kerry baada ya kikosi chake kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Mapinduzi Cup January mwaka huu.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top