FAIDA AMBAZO UFARANSA INAPATA KWA KUWA NCHI MWENYEJI WA EURO 2016



Michuano ya Euro 2016 inayoendelea nchini Ufaransa inaleta mjadala mpana juu ya masuala ya kiulinzi nchini vilevile athari za moja kwa moja za kiuchumi
na kisiasa kwa serikali ya nchi hiyo.

Mashambulizi ya kigaidi ya Paris yaliyotokea Novemba 13 yalionesha namna gani kwamba tukio la walipuaji wa kujitoa mhanga walioingia kwenye uwanja wa “Stade de France” wakati wa mchezo kati ya Ufaransa na Ujerumani halikuwa la bahati mbaya. Magaidi waliuteka uwanja ambao June 10 Mashindano haya ya Ulaya yalizinduliwa na kuhitimishwa tena baadaye kwenye uwanja huo huo.

Tangu mashambulizi hayo kutokea, mamlaka mbalimbali za nchini humo zimekuwa zikiweka sana msisitizo kwenye idara ya ulinzi juu ya tukio hilo la kuhitimisha michuano hii. Lakini kama ambavyo Waziri Mkuu Manuel Valls amerudia kwa kusema kwamba hakuna sababu ya kuwa na hofu yoyote licha ya magaidi wa IS kudai kwamba wana mpango wa kurudia kufanya mlipuko.

Tishilo hilo la kigaidi linaweza kuleta athari kubwa kwa taifa hilo kwenye tukio hilo maalum ambalo linaweza kuleta faida kubwa ya kiuchumi kwa nchi.

Changamoto ya ulinzi

Tangu kutokea kwa shambulizi hilo Novemba mwaka jana, idara za ulinzi zimekuwa zikikosolewa mara kwa mara kwa namna zinavyolishughulikia tishio hilo la kigaidi. May 21 mfumo wa ulinzi wa uwanja wa Stade de France ulipitiwa upya ili kufanyiwa marekebisho kwenye mchezo wa Kombe la ligi kati ya PSG na Marseille (mchezo ambao kiasili una uhasimu mkubwa), wakati mashabiki walipopiga baruti na kurusha mafataki uwanjani.



Onyo hilo limepuuzwa na mamlaka za nchini Ufaransa, ambazo zinadai kwamba mashabiki waliofika hapo wana asili tofauti-tofauti na wasimamizi na waendeshaji wa michuano hii (Uefa, badala ya Shirikisho la Soka Ufaransa kwenye mchezo wa Paris-Marseille) wana jukumu la kudhibiti kila kitu. Hata hivyo kwenye mchezo kati ya England na Russia kwenye wiki ya kwanza kabisa ya mashindano ilishuhudiwa vurugu zikitokea uwanjani na majukwaani na kuzidi kuleta sintofahamu juu ya uimara wa vifaa vya ulinzi uwanjani hapo.

Kiukweli, mfumo wa kisasa wa ulinzi uliowekwa kwasababu ya kulinda mashabiki dhidi ya magaidi na wahalifu. Ufaransa bado iko chini ya hali ya hatari na inaweza kufunga mipaka yake na kufanya operesheni ya haraka dhidi ya tishio lolote likalithibitika. Mahusiano kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani, UEFA na Jeshi la Polisi la Kupambana na Wahalifu Ulaya yalitakiwa kuimarishwa, na Ufaransa itasambaza nchi nzima zaidi ya maafisa wa polisi 70 000, walinzi 12 000 na wanajeshi 10 000 ili kuimarisha ulinzi.

Njia nyingine ni zile zinazojumuisha wataalam maalum wa uchambuzi watakaokuwa wanafuatilia kwa makini vitisho kwa kuangalia tathmini ya skeli ya tukio kuanzia 1 mpaka 4 kwenye kila mechi, perimeta za ulinzi mbili-mbili kwenye kila eneo la uwanjani, na kuweka vifaa maalum majukwaani vitakavyoweza kuangalia kila tukio linaoendela na kuonekana nchi nzima. Hii itasaidia kupunguza ukosoaji kutoka kwa wapinzani kwa kile wanachodai ni kukosekana kwa watu waliobobea kwenye masuala ya ulinzi hasa kutoka sekta binafsi.

Unions lock-up

Wakati huo huo, wanapaswa kutatua mgogoro mwingine mzito, kutokana na muungano wa watu mbalimbali kutishia kufanya mgomo endapo kama Paris itakataa kufanya marekebisho ya kwenye maslahi ya wafanyakazi.

Nchi imekuwa ikiandamwa na migogoro katika nyanja ya usafiri na vyama vya ushirika vimetangaza kuweza kuifunga nchi ikiwa serikali itagoma kutoa suluhulisho la namna ya kufanya makubaliano miongoni mwa makampuni badala ya kufanya kwa kuangalia matakwa yao binafsi.



Mjadala juu ya marekebisho umegawanya jamii ya wafaransa, na matumizi ya amri 49-3-ambayo inawazesha serikali kulazimisha mswada kupitia bungeni imeufanya mjadala kuwa na fukuto. Kama serikali inabaki na msimamo wake na vyama vya ushirika vikatoa vitisho, ushindani utasababisha mpasuko katika jamii ambao utapelekea vitendo vya hujuma kuelekea tukio muhimu lenye mustakabali mkubwa wa kiuchumi kwa Ufaransa.

Fursa za Kiuchumi

Kimsingi, Michuano ya Euro ni tukio kubwa la tatu la kimichezo duniani kwa maana ya kubeba hisia kubwa za vyombo vya habari na manufaa ya kiuchumi, baada ya Michuano ya Olimpiki na Kombe la Dunia. Kwa mujibu wa Kituo cha Uchumi wa Michezo na Sheria cha Limoges, tukio hili tayari limetengeneza kazi 20,000 na inaweza kusababisha mapato kupanda mpaka kiasi cha euro bil 1.4 (sawa na dola bil 59).

Mbali na faida ya moja kwa moja inayotokana na mapato ya viingilio, faida ya uwepo wa mashabiki na mapato mengine yanayohusiana na tukio hili, michuano hii pia italeta athari chanya za kiuchumi katika sekta ya utalii, ambayo inachukumia asilimia 7.4 ya uchumi wa Ufaransa. Mafanikio ya tukio hili yataongeza ufanisi kwenye sekta hiyo ambayo iliathirika vikali kutokana mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 2015, kwa kuondoa hofu kwa watalii.

Serikali ya Ufaransa pia imeweka mkazo mkubwa kwenye tukio hilo kama sehemu ya fursa ya kuitangaza nchi kimasoko hasa sekta ya utalii kwenye majiji ambayo huwa hayana mvuto kwa watalii wengi kama Northern town Lens. Zaidi ya hapo, jiji la Paris linatumaini kutumia Euro kama jukwaa la kampeni ya kuandaa Michuano ya Olimpiki mwaka 2024.

Vilevile, serikali itatumia tukio hili na vyombo vya habari kujitangaza kwenye masuala ya kidiplomasia kutokana na kuiona fursa kubwa ya kutangaza machapisho mbalimbali. Kwenye mechi kati ya Poland na Ujerumani iliyopigwa June 16, viongozi wa nchi hizo walikaa pamoja na wenzao wa Ufaransa kujadili masuala ya utawala wa sheria, wiki kadhaa baada ya Brussels kuchapisha maoni hasi juu ya kitendo cha Warsaw kuipokonya nguvu mahakama kuu.

Fursa kwa Hollande

Mwisho kabisa, rais wa Ufaransa anaweza kuhesabu Michuano ya Euro kama mafanikio tosha ya madai kwamba mambo yanazidi kuwa mazuri nchini. Kimsingi ongezeko la faida kwenye robo ya kwanza ilikuwa bora zaidi ya ilivyotarajiwa (0.6% badala ya 0.5%) na uwekezaji katika biashara umeongezeka kwa kasi hadi 2.4% badala ya 1.6% ilivyokadiriwa hapo mwanzo. Idadi ya kazi pia imeongezeka ndani ya miezi miwili mfululizo, huku malalamiko watu wasio na kazi yakizidi kupungua.



Licha ya kuimarika kwa kiasi kikubwa hivi karibuni, umaarufu wa rais unazidi kushuka. Kwa mujibu wa savei iliyofanywa na Taasisi ya utafiti ya Cevipof, ni asilimia 4 tu ya wananchi ambao wanaridhishwa na rais, na 14% wamempigia chapuo ya kuendelea kugombea uchaguzi ujao, suala ambalo linatoa ugumu kwake kuwa na vigezo vya kupambana kwenye mbio hizo.

Ikiwa Ufaransa watashinda ubingwa huu, itamsaidia kwa kiassi kikubwa kuleta kwa mdahalo wa wazi, na vilevile kupunguza hofu kwa wananchi. Ikumbukwe hapo awali kulikuwa na vuguvugu juu ya kuwepo kwa upendeleo kwenye uteuzi wa wachezaji kwenye timu. Ilidaiwa kwamba uteuzi uligubikwa na ubaguzi wa rangi kuliko kuangalia uwezo wa wachezaji. Karim Benzema alikuwa moja ya wachezaji waliohusishwa na sakata hilo. Benzema alikuwa anashutumiwa kwa kutishia kuvujisha video za ngono za mchezaji mwenzake. Lakini baadaye kocha wa Ufaransa alishutumiwa na mashabiki kwamba alipata msukumo kutoka kwa kundi moja la nchini Ufaransa linalojihusisha na masuala ya kibaguzi.

Mjadala wa ubaguzi wa rangi ni hoja kuu ya Chama cha Nationa Front ambacho ni mrengo wa watu wasiopenda wahamiaji (na wasiopenda Umoja wa Ulaya) na ambacho kinanufaika kwa kuona kuna mpasuko kwenye jamii hasa kwenye suala kama hili. Mwisho wa siku, ushindi wa Ufaransa kwenye michuano hii utadumisha mshikamano kuelekea mustakabli mpya wa kujenga taifa linaoundwa kwa pamoja na watu weusi, wazungu wenyewe na wachezaji kutoka mataifa ya Afrika Kaskazini kama ilivyokuwa wakati ule walivyoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top