MASTAA 9 AMBAO MICHUANO YA EURO IMEPANDISHA NA KUSHUSHA THAMANI ZAO


Kwa namna miaka ya hivi karibuni vilabu vinavyotafuta wachezaji, ni vigumu sana mchezaji ambaye hajulikani na pengine akafanya mambo makubwa kwenye michuano fulani mikubwa kwa mfano Euro
au Copa America na ghafla kununuliwa na timu kubwa.

Hata hivyo uwezo binafsi wa mchezaji husika walau unaweza kupandisha thamani yake katika soko la usajili ama kushusha kabisa thamani yake.

Wafuatao ni wachezaji ambao kupitia michuano ya Euro mwaka huu thamani yao inaweza kuwa imepeanda na baadhi yao kushuka.

Wachezaji ambao thamani yao imepanda

Moussa Sissoko

Sidhani kama kuna yeyote aliyeifuatilia kwa uzuri michuano ya Euro kama atabisha juu ya hili. Sissoko amekuwa na kiwango cha hali ya juu katika michuano hii na naamini hata timu yake ya Newcastle itashangaa, kwamba uwezo wa mchezaji wao huyu ulijificha sehemu gani kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Naamini vilabu mbalimbali vitaanza kumfuatilia ili kunasa saini yake. Amecheza mpira mkubwa sana kwenye michuano ya Euro hasa katika mechi ya fainali dhidi ya Ureno licha ya timu yake kupoteza mchezo.

Kwa namna moja ama nyingine anaamini Sissoko hatabaki Ligi daraja la Kwanza England ambapo timu yake itakuwa ikishiriki baada ya kushuka daraja msimu uliopita.

Joao Mario

Mreno huyu ama hakika amekuwa kwenye kiwango bora kabisa kwenye michuano ya Euro mwaka huu. Joa Mario ambaye kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Sporting Clube de Portugal (Sporting Lisbon) ya nchini Ureno.



Uwezekano mkubwa wa kupaa kwenda kwenye ligi mbalimbali kubwa kama England na Uhispania endapo vilabu mbalimbali vimemtupia jicho la tatu. Tayari kuna tetesi za klabu ya Inter Milan kuanza kumnyemelea kwa dau la euro milioni 50.

Ivan Perisic

Licha ya timu yake ya Croatia kutolewa katika hatua ya 16 bora na Ureno, lakini hakuna shaka kwamba uwezo wa Perisic ulikuwa ni wa hali ya juu kabisa. Alicheza vyema kuanzia mwanzo wa mashindano mpaka pale waliotolewa.



Ivan Perisic 

Alifunga goli muhimu la ushindi kwenye mchezo dhidi ya Uhispania ambapo Croatia walishinda magoli 2-1 na kuongoza kundi. Kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Inter Milan lakini muda wowote anaweza kuondoka kuelekea kwenye vilabu vyenye hadhi zaidi.

Robbie Brady

Kabla ya Michuano ya Euro mwaka huu kuanza, Brady alitoka kupata machungu baada ya timu yake ya Norwich City kushuka daraja. Alifunga goli muhimu la ushindi dhidi ya Itlay katika hatua ya makundi na goli la penati dhidi ya Ufaransa. Amekuwa akihusishwa kwa karibu kutakiwa na klabu ya Leicester City na pengine kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi anaweza kuwa amekamilisha dili hilo. Ni mchezaji anayesifika kwa upigaji mzuri wa mipira ya adhabu pamoja na kona.

Hal Robson-Kanu

Thamani yake ilikuwa ya chini sana kabla ya Michuano ya Euro mwaka huu kutokana na kuwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na klabu yake. Lakini uwezo wake kwenye timu ya taifa ya Wales umewashtua wengi. Goli lake muhimu dhidi ya Ubelgiji ni alama tosha ya ubora wake.
Tayari klabu ya Hull City imeanza mikakati ya kunasa saini yake licha ya kupata ushindani kutoka vilabu vya Beijing Guoan na Jiangsu Sunning kutoka China ambavyo vimemuahidi ofa ya mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki.Wachezaji ambao thamani yao imeshuka



Arda Turan

Kabla ya Michuano ya Euro hakuwa kwenye kiwango bora kwenye klabu yake ya Barcelona. Michuano ya Euro ndiyo imezidi kuporomosha thamani yake kabisa. Ndiyo nahodha wa Uturuki lakini alishuhudia timu yake ikipoteza mechi mbili na kuibuka kwenye mchezo wa mwisho na kushinda. Baadaye aliomba radhi kwa mashabiki wao kwa kiwangokibovu cha timu yao. Kwa sasa Arda hawezi kutakiwa na klabu yoyote kubwa duniani kutokana na namna alivyoonesha kiwango chake katika siku za hivi karibuni.



Mario Gotze

Kama una kumbukumbu nzuri, huyu ndiyo mchezaji aliyefunga goli la ushindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka juzi dhidi ya Argentina. Kwenye klabu yake ya Bayern alikuwa hapewi nafasi kubwa katika msimu uliomalizika, na mbaya zaidi kwenye Michuano ya Euro ndipo alizikwa kabisa. Kocha wake alipenda kumtumia Mario Gomez kutokana na kuamua kutotumia tena mfumo uliokuwa ukimpa nafasi.


Alipewa nafasi kweye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ufaransa lakini hakufanya lolote. Liverpool, Borussia Dortmund na Tottenham Hotspurs wametajwa kumnyemelea, lakini kwa kiwango hiki alichoonesha inawezekana vilabu hivyo vikasitisha mipango yao ya kumnyaka.

Wayne Rooney 

Kocha wake wa sasa kunako klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema hatamtumia katika nafasi ya kiungo badala yake atampa nafasi ya ushambuliaji.




Na hii pengine imechangiwa na kiwango alichoonesha kwene Michuano ya Euro. Amekuwa mzuri katika kupiga pasi ndefu na sio kufumania nyavu tena. Timu yake ya England ilitolewa kwa aibu na timu changa ya Iceland kwa kufungwa magoli 2-1.

Adil Rami

Alianza vyema kwa kupewa nafasi ya kucheza kwenye Michuano ya Euro akiwa na timu yake ya Ufaransa. Baadaye alipata adhabu iliyomweka nje na na nafasi yake kuchukuliwa na Samuel Umtiti. Umtiti alikaba kabisa nafasi ya Rami na kuondoa nafasi yake ya kutazamwa na vilabu vikubwa. Kwa sasa anakipiga na Sevilla na pengine ataendelea kubaki pale kutokana na kutokuwa na vilabu vyovyote kutajwa kumnyemelea.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top