Mashabiki wa Yanga wakimkabidhi Haji Manara mchango kwa ajili ya Matibabu (Picha na Godlisten Chicharito)
Wanachama na mashabiki wa klabu ya Yanga wakiongozwa na Jerry Muro wamemtembelea mkuu wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Bw. Haji Manara na kumkabidhi mchango wao kwa ajili ya matibabu ya jicho lake ambalo limepoteza uwezo wa kuona.
Wanazi hao wa Yanga walifika nyumbani kwa Manara na kutoa mchango wao ambao walichanga kupitia makundi mbalimbali ya kwenye mitandao ya kijamii.
Manara anatarajiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali katika hospitali kadhaa za hapa nchini.
Msemaji huyo wa wekundu wa Msimbazi amesema gharama kwa ajili ya matimu zinakadiriwa kuwa ni zaidi ya dola 10,000 za Marekani.
Manara amewashukuru mashabiki hao kutokana na moyo wao wa kiungwana wa kumtembelea kwa ajili ya kumsalimia na kumjulia hali lakini pia kukabidhi mchango wao katika jitihada za kuhakikisha anapata matibabu.
“Mimi niwashukuru sana kwa mchango wenu, mnaweza mkakakiona kidogo lakini hakuna kidogo katika tiba. Ni kweli gharama ya matibabu ni kubwa ni zaidi ya dola 10,000 lakini hiki kitakuwa ni sehemu kitakuwa ni sehemu ya mchango mkubwa, kwanza si kwa suala la kiasi lakini ni kwasababu kimetoka kwa watu ambao wameonesha utamaduni unaotakiwa,” alisema Manara wakati akitoa shukrani kwa mashabiki wa Yanga waliomtembelea nyumbani kwake.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)