Breaking news: Theresa May ndiye waziri mkuu wa Uingereza




Theresa May ndiye waziri mkuu wa Uingereza

Bi Theresa May amechukua usukani kama waziri mkuu wa Uingereza.

Akizungumza baada ya kupokea ufungua wa makao rasmi ya waziri mkuu wa Uingereza 10 Downing Street bi May amehakikishia washirika wake na
mataifa ya muungano wa ulaya kuwa licha ya taifa hilo kuamua kujiondoa,

Uingereza inapania kujiunga na mataifa shirika na kutekeleza wajibu wake katika muungano wa mataifa huru duniani.

Amesema kuwa serikali yake haitanaswa na mtego wa kuwasikiza mabwenyenye walio wachache na kusahau wananchi wa kawaida. Malkia tayari amempa idhini ya kuunda serikali mpya muda mchache tu baada ya kujiuzulu rasmi kwa aliyekuwa waziri mkuu bwana David Cameron.

May amesema kuwa serikali yake itahakikisha inawakilisha matarajio ya kila muingereza.

Aliwakumbusha wakosoaji wake maana ya jina rasmi ya chama chake ambacho ni chama cha Conservative and Unionist.

Waziri huyo mkuu ameapa kuangamiza udhalimu wa aina yeyote ima ni kwa misingi ya ubaguzi wa rangi jinsia ama kiwango cha mapato.

Bi Theresa May ni waziri mkuu wa 13 kuwahi kuiongoza Uingereza katika enzi ya Malkia Elizabeth wa pili. Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuhudumu kama waziri mkuu tangu Margaret Thatcher.

Malkia tayari amempa idhini ya kuunda serikali mpya muda mchache tu baada ya kujiuzulu rasmi kwa aliyekuwa waziri mkuu bwana David Cameron.

Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuhudumu kama waziri mkuu tangu Margaret Thatcher.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top