Cristiano Ronaldo kuwa mwanasoka bora katika tuzo ya mchezaji bora Ulaya 2015/2016?

Ronaldo alishinda Euro 2016 akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno


Shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza majina ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya kwa msimu wa mwaka 2015/2016, majina hayo 10 yametangazwa huku Cristiano Ronaldo akipewa
nafasi ya kushinda tuzo hiyo itakayotolewa Agosti 25 mwaka huu.

Majina hayo 10 yametangazwa baada ya kufanyika mchujo wa majina ya wachezaji 37 ambao walikuwa wamependekezwa awali na kupigiwa kura, ambapo UEFA imetaja majina ya wachezaji 10 waliofanikiwa kuingia katika kumi bora ikiwa majina 27 ya wachezaji yaliingia katika kinyanga’nyiro hicho.

Majina ya wachezaji hao kumi ni Gareth Bale – Real Madrid, Gian-luigi Buffon -Juventus , Antoine Griezmann - Atletico Madrid, Toni Kroos - Real Madrid , Lionel Messi -Barcelona, Thomas Müller -Bayern Munich, Manuel Neuer - Bayern Munich , Laveran Ferreira Pepe - Real Madrid, Cristiano Ronaldo -Real Madrid, Luis Suarez –Barcelona.

Mshirikishe mwenzako

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top