KUHUSU WANACHUO WALIOKUWA WANASOMA STASHAHADA MAALUM YA UALIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA

[​IMG]

TAARIFA KWA UMMA 



1.0 UTANGULIZI
Itakumbukwa kwamba tarehe 28 Mei, 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati Chuo Kikuu Dodoma. Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na mgomo wa walimu uliokuwa Orodha ya majina ya wanchuo watakaorudi kusoma Udom bofya hapa
umedumu kwa takribani wiki 3. Wanafunzi waliosimamishwa masomo walikuwa wamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza lilikuwa ni wanafunzi 6,595 waliodahiliwa katika Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari na kundi la pili lilikuwa na wanafunzi 1,210 waliodahiliwa katika mafunzo ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi. 

2.0 SIFA ZA KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA STASHAHADA

Baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa, Serikali ilifanyaUchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao. Sifa zilizotakiwa ni ufaulu wa Daraja la I hadi la III na credit mbili au zaidi katika masomo ya Sayansi na Hisabati.Mchanganuo wa ufaulu wa Kidato cha Nne kwa wanafunzi hao 
Chanzo: Baraza la Mitihani Tanzania

Jedwali Na. 1 linaonesha kuwa kulikuwa na wanafunzi 52 waliopata Daraja la IV kinyume na matakwa ya Programu ambapo mwanafunzi alitakiwa awe na ufaulu wa Daraja la I – III. Aidha, uchambuzi zaidi ulifanyika kwa wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la I-III ili kujiridhisha kama wamekidhi kigezo cha kuwa na ufaulu katika masomo mawili kwa kiwango cha C-A.

3.0 UCHAMBUZI WA SIFA ZA WANAFUNZI

Uchambuzi wa sifa kwa kuzingatia vigezo vya kujiunga vilivyowekwa umebainisha yafuatayo:

1. Wanafunzi 6,595 walidahiliwa kusoma programu ya Stashahada Maalum ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari kwa Masomo ya Hisabati na Sayansi.Kati yao,6305 walikuwa na sifa stahiki ambazo ni ufaulu kwa Daraja la I – III na ufaulu kwa kiwango cha gredi C-A katika masomo mawili ya Sayansi. 



Wanafunzi 4,720 walikuwa mwaka wa kwanza na wanafunzi 1,585 walikuwa mwaka wa pili. Mchanganuo wa ufaulu wao umeainishwa katika Jedwali Na. 2.

Jedwali 2: Ufaulu wa Wanafunziwa Stashahada ya Ualimu Sekondari Waliokidhi Vigezo vya Udahili


2. Wanafunzi 290 hawakuwa na sifa za kudahiliwa kwenye Programu maalum ya ualimu wa Shule za Sekondari. Matokeo ya Kidato cha Nne ni kama ifuatavyo:

Jedwali linaonesha kuwa:

a) Wanafunzi 21 walikuwa na ufaulu wa Daraja la IV wakati walipaswa kuwa na Daraja la I - III;

b) Wanafunzi 269 walikuwa na ufaulu wa kati ya Daraja la I-III (II – 9; III - 260) lakini hawakuwa na Ufaulu wa kiwango cha C-A kwa masomo mawili ya Sayansi.

3.1 Programu ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi 

Uchambuzi wa sifa ulifanyika pia kwa wanafunzi 1,210 waliokuwa wamedahiliwa katika Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi na kubaini yafuatayo:

(i) Wanafunzi 29 wa mwaka wa II walikuwa ni walimu wa shule za msingi ambao walikuwa wamehitimu Kidato cha Nne na kuhudhuria mafunzo ya Ualimu wa Cheti (Daraja la IIIA) ambao walikuwa na uzoefu kazini wa miaka miwili au zaidi. Mchanganuo wa matokeo yao ya Kidato cha Nne umeainishwa katika jedwali lifuatalo:
(ii) Wanafunzi 1,181 walikuwa ni wahitimu wa Kidato cha Nne ambao mchanganuo wa matokeo yao ya Kidato cha Nne umeainishwa katika Jedwali lifuatalo:


Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (Mb)

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

19 Julai, 2016


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top