Venezuel, Mexico zatinga robo fainali Copa America, Tazama ratiba ya leo

Solomon Rondon ameiwezesha Venezuela kutinga hatua ya robo fainali, baada ya kuifungia timu yake bao pekee dhidi ya Uruguay kwenye mchezo wa kundi C. Rondon alifunga bao hilo kunako dakika ya 36 ya mchezo akiuwahi mpira ulimbabatiza mlinda lango wa UruguayFernando Muslera na kugonga mwamba kufuatia shuti kali lililopigwa na kiungo Alejadro Guerra.


Mshambulizi Edison Carvan alikosa nafasi nyingi za kufunga ikiwemo moja aliyobaki yeye na kipa Jose Contreras wa Venezuela.
Katika mechi ya pili Mexico iliichapa Jamaica kwa mabao 2-0 na kutinga hatua ya robo fainali. Ikicheza kwenye uwanja wa Pasadena Rose Bowl na kushuhudiwa na watazamaji wapatao 63, 263, iliwachukuwa Mexico dakika 18 kujipatia bao lililowekwa kimiani na Chicharito kwa kichwa akiunganisha krosi ya Jemenez.


Hilo likawa bao lake la 45 kwa timu yake ya taifa.Kunako dakika ya 65 mchezaji Donaldson wa Jamaica aliangushwa ndani ya sanduku la penati lakini kwa mshangao wa watazamaji wengi mwamuzi alipeta na kuwafanya Jamaica kulalamika sana. Dakika ya 81 Oribe Peratta aliipatia Mexico bao la pili na kufanya matokeo yasomeke 2-0 mpaka mwisho wa mchezo.
Baadaemichuano ya leo ni
CHILE vs BOLIVIA
PANAMA vs ARGENTINA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top