Michuano ya Euro mwaka 2016 inaanza rasmi leo kwa mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Ufaransa dhidi ya Romania kwenye uwanja wa Stade de France.
Kuelekea michuano hiyo, hii ndiyo rekodi ambayo inamaajabu ndani yake, timu ambayo ilicheza fainali ya kombe la dunia na kupoteza mchezo huo halafu ikaelekea kwenye michuano ya Euro ilitolewa kwenye hatua za mwanzo kabisa.
Angalia rekodi kisha tusubiri nini kitatokea kwenye michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa
Tangu 1996, Euro ilipoanza kushirikisha timu 16, timu iliyofungwa fainali ya kombe la dunia lililopita kabla ya Euro husika, ilitolewa raundi ya kwanza ya Euro.
Euro 1996, Italia walifungwa fainali ya kombe la dunia 1994. Euro iliyofuata ilikiwa Euro 1996, walitoka raundi ya kwanza.
Euro 2000, waliofungwa fainali ya kombe la dunia 1998 ni Brazil (hawashiriki Euro)
Euro 2004, Ujerumani walifungwa fainali ya kombe la dunia 2002. Euro iliyofuata ilikuwa mwaka 2004, Ujerumani walitolewa raundi ya kwanza.
Euro 2008 Ufaransa walifungwa fainali kombe la dunia 2006. Euro iliyofuata ilikuwa 2008, walitolewa raundi ya kwanza.
Euro 2012 Uholanzi walifungwa fainali ya kombe la dunia 2010. Euro iliyofuata ilikuwa Euro 2012, walitolewa raundi ya kwanza.
Tuone Euro ya muundo mpya, Euro 2016, itakuja na maajabu gani?