Maradona na Pele wadukuliwa wakimjadili Messi
Aliyekuwa nyota wa soka nchini Argentina, Diego Maradona, na gwiji mwingine wa soka Pele wamesikika wakijadili umaarufu wa mshambuliaji nyota wa Argentina na Barcelona Lionell Messi.
Maradona alisema Messi ni mtu mzuri na mchezaji hodari lakini hana tajiriba ya kuwa kiongozi.Wawili hao walikutana mjini Paris Ufaransa siku moja tu kabla ya kuanza kwa mechi za kuwania kombe la taifa bingwa barani Ulaya Euro2016.
Pele naye alionekana kukubaliana naye.
Wawili hao walikutana mjini Paris Ufaransa siku moja tu kabla ya kuanza kwa mechi za kuwania kombe la taifa bingwa barani Ulaya Euro2016.
Shirikisho la mchezo wa soka duniani, FIFA limewataja Pele na Maradona kama wachezaji waliotia fora sana katika soka duniani.