PICHA 9: HALI ILIVYO UWANJA WA TAIFA KUELEKEA YANGA VS MAZEMBE

Leo pale taifa unachezwa mchezo wa kombe la shirikisho Afrika kati ya mabingwa wa Tanzania Young Africans dhidi ya TP Mazembe mabingwa wa DR Congo ukiwa ni mchezo wa pili kwa timu zote mbili.

Mchezo huo umekuwa na mambo mengi sana nje ya uwanja kitu ambacho kinazidi kuwafanya wadau wengi wa soka la bongo kutamani kuona na hata kujua ni nini kitatokea uwanjani ndani ya saa moja na nusu ya mchezo huo (dakika 90).

Uongozi wa Yanga umetangaza kuwa hakutakuwa na kiingilio kwenye game hiyo, sasa kilichotokea ni kufurika kwa mashabiki uwanjani kuanzia asubuhi wakianza kuingia uwanjani wakihofia kukosa nafasi itakapofika majira ya mchana.

Hali ilivyo asubuhi hii na kama una mpango wa kuushuhudia mchezo huo uwanjani basi utakuwa unajua unatakiwa kufanya nini mida hii.


Uingereza yatolewa michuano ya EURO 2016 Bofya hapa



News alert: Chile yatwaa Ubingwa tena Copa America Bofya hapa
Video: MESSI AKOSA PENATI NA KUISHUHUDIA CHILE IKITWAA UBINGWA COPA AMERICA bofya hapa 


Breaking news: Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa bofya hapa 







Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top